Jinsi Tunavyoweza Kusaidia
Huduma za Kisheria za Vermont na Vermont Legal Aid hutoa usaidizi wa kisheria wa kesi za kiraia (si za jinai) kwa wakaaji wa Vermont wenye mapato ya chini. Huduma zetu ni bure.
Huduma za Kisheria za Vermont huchunguza maombi yote ya usaidizi wa kisheria. Ikiwa tunaweza kusaidia katika tatizo la kisheria, tutakuelekeza kwa wanasheria na mawakili wetu au tutakuelekeza kwa wanasheria na mawakili walio katika Usaidizi wa Kisheria wa Vermont (Vermont Legal Aid). Pia tunaweza kukuelekeza kwa mipango mingine.
Wasiliana nasi ili ujue ikiwa tunaweza kukusaidia. Tunaweza kukupa ushauri. Tunaweza kukuambia mahali pa kupata taarifa ya kukusaidia kujiwakilisha mahakamani.
Hatuwezi kusaidia kila mtu anayehitaji msaada. Huenda tusiweze kukusaidia kulingana na mapato yako. Hatuna wanasheria wa kutosha wa kusaidia kila mtu anayetuomba usaidizi.
Jinsi ya kuwasiliana nasi
Piga simu namba ni 1-800-889-2047 na uache ujumbe, au utumie Fomu yetu ya Ombi la Usaidizi wa Kisheria ya mtandaoni.
Ikiwa huzungumzi Kiingereza, omba huduma ya mkalimani. Tutakupatia mkalimani bila malipo.
Ofisi zetu zinafunguliwa Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 8:30 asubuhi hadi saa 4:00 jioni.
Huwa tunapata maombi mengi ya usaidizi. Usingoje hadi dakika ya mwisho ili utupigie simu kuhusu tatizo la dharura!
Usisahau kutuambia nambari yako ya simu na utufahamishe wakati mzuri wa kukupigia simu tena. Tafadhali endelea kusubiri simu yetu. Utapigiwa simu kutoka kwa nambari ya simu ya 802 ambayo labda hauitambui!
Jinsi tunavyofanya kazi
Tutakuuliza maswali machache ili kubaini ikiwa unastahiki kuzungumza na mojawapo wa mawakili wetu. Hii inaitwa "mchakato wa kuandikishwa".
Kwa mfano, tutakuomba:
- taarifa za kibinafsi kama vile anwani yako, nambari ya simu, umri wako, ikiwaumeolewa au umeoa, na idadi ya watu wanaoishi nawe
- maelezo ya tatizo au suala ambalo unawasiliana nasi kulihusu
- kiasi cha mapato na mali yako ili kubaini ikiwa tunaweza kukusaidia
Taarifa yote unayotuambia inalindwa. Haitashirikiwa bila idhini yako.
Wafanyakazi wetu wataamua jinsi bora ya kukusaidia
Kulingana na hali yako na ikiwa unastahiki kwa usaidizi, unaweza kupata:
- ushauri wa kisheria kupitia simu
- taarifa kwenye barua ya posta au barua pepe
- utafiti finyu wa kisheria
- kuelekezwa kwa mwanasheria au wakili ili akusaidie
- kuelekezwa kwa shirika lingine, au
- kuelekezwa kwa wakili binafsi
Tafadhali jua kwamba: Hatuwezi kukusaidia na matatizo ya ukiukaji wa sheria za barabarani. Hatuwezi kukusaidia katika kesi nyingi za majeraha ya kibinafsi na sheria ya mali isiyohamishika. Pia hatuwezi kukutetea katika kesi ya jinai. (Hata hivyo, tunaweza kukusaidia ikiwa unahitaji usaidizi wa kisheria kutokana na kuwa mwathiriwa wa uhalifu.)
Je, huduma za kisheria za raia ni nini?
Vermont Legal Aid (Usaidizi wa Kisheria wa Vermont), Huduma za Kisheria za Vermont na mashirika mengine ya usaidizi wa kisheria yamejitolea kusaidia na kuwawakilisha watu katika maswala ya kisheria. Haya ni mashtaka na mashauri mengine ya kisheria yasiyohusiana na uhalifu.
Kwa mfano, kesi za kisheria za raia ni pamoja na migogoro mingi ya mwenye nyumba na mpangaji, kufilisika, masuala ya kadi ya mkopo, ubaguzi, kesi za Manufaa Reach Up na Usalama wa Kijamii na matatizo mengine kama hayo.
Watetezi wa Umma na mashirika mengine husaidia na kuwakilisha watu wanaohusika katika kesi ya jinai, ambayo ni wakati serikali inamshtaki mtu kwa kufanya kitendo cha jinai.
Je, wewe ni mwathiriwa wa uhalifu?
Iwapo una tatizo la kisheria kwa sababu ya kuwa mwathiriwa wa uhalifu au unyanyasaji, tembelea ukurasa wetu wa Usaidizi wa Kisheria kwa Waathiriwa wa Uhalifu ili uone jinsi tunavyoweza kukusaidia.