Sheria ya CARES – COVID-19 Malipo/Hundi ya Kujikimu ya Athari za Kiuchumi za Virusi vya Korona
Imesasishwa Aprili 16, 2020
Sheria ya msaada wa virusi vya korona ya serikali kuu (inayoitwa sheria ya CARES) itatoa fedha kwa watu wazima wengi nchini Merikani. IRS itatuma fedha kwenda nyumbani kwako au itaweka kwenye akaunti yako ya benki. Baadhi ya watu ambao hawajawasilisha malipo ya kodi wanapaswa kuwasilisha fomu ya kodi ili kupata fedha hiyo. IRS inasema kwamba uwekaji fedha kielektroniki kwa Malipo ya Athari ya Kiuchumi ya serikali kuu (EIP) utaanza karibia Aprili 13, 2020.
Jihadhari na matapeli!
Tunahofia juu ya uwepo wa utapeli na udanganyifu kutokana na ujio wa malipo ya kujikimu. Usitoe taarifa zako binafsi au namba ya akaunti ya benki kwa mtu yeyote ambaye anasema unaweza kupata fedha za malipo ya mapema ya fedha hizi. Usijaze maombi yeyote ya kupata fedha zako haraka. Mfumo haufanyi kazi hivyo.
IRS haita kupigia simu, haita kutumia ujumbe, barua pepe au kuwasiliana na wewe kwa njia ya mitandao ya kijamii kukuomba taarifa zako binafsi au akaunti ya benki — hata inayohusiana na malipo ya athari za kiuchumi. Pia, jihadhari na barua pepe zenye viambatisho au viunganishi zikidai kuwa zina taarifa maalum kuhusu malipo ya athari za kiuchumi au kurejeshewa fedha. Usifungue barua pepe na usibofye kwenye viambatisho wala viunganishi. Nenda kwenye IRS.gov kwa taarifa zaidi kuhusu utapeli.
Maelekezo
Kama umewasilisha malipo ya kodi ya 2018 au 2019, utapata moja kwa moja EIP yako kwa kuweka fedha moja kwa moja au hundi kutegemeana na jinsi ulivyowasilisha kwa ajili ya kurejeshewa fedha katika miaka hiyo ya kodi. Hutakiwi kufanya chochote.
Ikiwa hukuwasilisha malipo ya kodi ya 2018 au 2019, lakini unapokea Hifadhi ya Jamii, Hifadhi ya Jamii ya Ulemavu (SSDI) au Kustaafu katika Njia ya Reli, utakuwa umepata fomu ya kodi inayoitwa SSA-1099 au RRB-1099 Januari au Februari. Kwa hali hii, utapata hundi yako ya kujikimu moja kwa moja. Hutakiwi kufanya chochote. Kama wewe ni mnufaika wa Mapato ya Ziada ya Usalama (SSI) , utapata hundi ya kujikimu moja kwa moja. Hutakiwi kufanya chochote. (Angalia maelezo hapo chini iwapo umeanza kupata Hifadhi ya Jamii au SSI mwaka 2020.)
Ikiwa hauhitajiki kuwasilisha malipo ya kodi, kama vile familia yenye kipato cha chini ambazo kipato chao ni chini $12,200 ($24,400 kwa wanandoa), au chanzo chenu pekee cha mapato ni Reach Up (TANF), Msaada wa Jumla au Mafao ya Uzeeni, IRS imeunda kituo cha mtandaoni kwa ajili yako ili kukupatia taarifa zako. Jaza fomu ya mtandaoni ili kupata hundi yako ya kujikimu. Taarifa unazohitaji kwenye fomu:
- jina kamili, anwani ya sasa ya posta na barua pepe
- tarehe ya kuzaliwa na namba halali ya Hifadhi ya Jamii
- namba ya akaunti ya benki, aina ya akaunti na namba kiunganishi, ikiwa una akaunti ya benki
- Namba ya Utambulisho Binafsi ya Kitambulisho (IP PIN) ikiwa umepata kutoka IRS mapema mwaka huu
- leseni ya udereva au Kitambulisho kilichotolewa na serikali, kama unavyo
- kwa kila mtoto anayestahili mwenye umri chini ya miaka 17 ambaye unaishi naye na anakutegemea: jina, Namba ya Hifadhi ya Jamii au Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi, na uhusiano wao kwako au mke mwanandoa mwenzio
Ikikiwa umeanza kupata mafao ya Hifadhi ya Jamii au ya SSI mwaka 2020, na hukuwasilisha malipo ya kodi ya 2018 au 2019, unaweza kutumia fomu hii hii ya mtandaoni ili kupata hundi yako ya kujikimu.
Pia, ikiwa mnufaika wa SSA -1099 au RRB-1099 (hiyo ni, mnufaika wa Hifadhi ya Jamii ya Kustaafu, SSDI au Ustaafu wa Njia ya Reli ) au mnufaika wa SSI, na una watoto wanaostahili wenye umri chini ya miaka 17 wanaoishi nyumbani, unaweza kutumia fomu hiihii moja ya mtandaoni kudai malipo ya $500 kwa kila mtoto.
Ikiwa unatakiwa kuwasilisha marejesho ya malipo ya kodi (kipato chanu cha mwako kilikuwa zaidi ya $12,200 au $24,400 kwa wanandoa), tumia huduma ya bure ya maandalizi ya kodi kama vile IRS Free File au Turbo Tax ili kujiandaa na kuwasilisha malipo ya kodi. Au unaweza kuwasilisha malipo ya kodi ya mapato kwa karatasi au tafuta mtaalam wa kuandaa kodi kupitia orodha hii.
Kumbuka, una hadi Julai 15, 2020, kuwasilisha malipo ya kodi. Malipo ya EIP yatatolewa hadi Desemba 2020.
Tutasasisha ukurasa wetu wa tovuti kwenye vtlawhelp.org pindi taarifa mpya inapoingia.
Angalia IRS.gov/coronavirus kwa taarifa zaidi.
Maswali na Majibu
Je, napaswa kufanya nini kuhusu udanganyifu na utapeli?
Tunahofia uwezekano wa udanganyifu na watu kukuibia. Hakuna mtu anayeweza kukusaidia upate hela hizi haraka. Usitoe taarifa zako za akaunti ya benki kwa mtu yeyote anayekwambia kwamba watakusaidia uzipate fedha zako. Hawawezi. Wanajaribu kukuibia. Nenda kwenye IRS.gov kwa taarifa zaidi kuhusu utapeli.
Je nitapata fedha kiasi gani?
Watu wazima ambao kipato chao ni chini ya $75,000/mwaka au wanandoa ambao kwa pamoja kipato chao kamili ni chini ya $150,000 watapata $1,200 kwa kila mtu mzima, jumlisha $500 kwa kila mtoto chini ya miaka 17 ambao wanaishi pamoja na wewe na wanakutegemea.
Kwa watu wenye kipato kikubwa, kiasi cha hundi ya kujikimu hupungua. Ikiwa unapata zaidi ya $99,000 au wanandoa ambao wanapata zaidi ya $198,000 hawatapata kiasi chochote cha fedha za kujikimu.
Je, nani anaweza kupata fedha za kujikimu moja kwa moja?
- Kila mtu mwenye Namba ya Hifadhi ya Jamii ambaye amelipa kodi ya 2018 au 2019
- Kila mtu ambaye ni mnufaika wa Hifadhi ya Jamii, Mapato ya Ziada ya Usalama (SSI), Bima ya Hifadhi ya Jamii kwa Wenye Ulemavu (SSDI), au ambaye anapata Mafao ya Uzeeni ya Njia ya Reli. (Lakini angalia maelezo hapo chini ikiwa umeanza kunufaika na Hifadhi ya Jamii au SSI mwaka 2020.)
Nani anatakiwa kuipatia IRS taarifa zaidi ili kupata fedha?
- Kila mtu ambaye hajawasilisha malipo ya kodi ya mwaka 2018 au 2019 na ambaye hajanufaika na Mafao ya Kustaafu ya Hifadhi ya Jamii au SSI au SSDI au Mafao ya Kustaafu ya Njia ya Reli
- Yeyote ambaye ananufaika na Hifadhi ya Jamii au SSI au SSDI na ana watoto au wajukuu wenye miaka chini ya 17 ambao wanaishi na wewe na wanakutegemea. Utatakiwa uwasilishe fomu ya kodi ili kupata $500 kwa kila mmoja wao.
- Yeyote ambaye ameanza kunufaika na Hifadhi ya Jamii au SSI mwaka 2020, na hakuwawasilisha malipo ya kodi ya 2018 au 2019
- Jaza fomu hii ya mtandaoni ya IRS.
- Ikiwa huna mtandao wa intaneti, unapaswa kuwasilisha kodi kwa njia ya karatasi. Hii itachukua muda mrefu kushughulikiwa na IRS.
Nani anatakiwa kuwasilisha malipo ya kodi ili apate fedha za kujikimu?
Ikiwa unatakiwa kuomba kurejeshewa malipo ya kodi (kipato chako cha mwaka kilikuwa zaidi ya $12,200 au $24,400 kwa wanandoa), unaweza kutumia huduma ya maandalizi ya kulipa kodi kama vile IRS Free File au Turbo Tax ili kujiandaa na kuwasilisha malipo ya kodi. Au unaweza kuwasilisha malipo ya kodi ya mapato au tafuta mtaalam wa kuandaa kodi kupitia orodha hii.
Kumbuka, una hadi Julai 15, 2020, kuwasilisha malipo ya kodi. Malipo ya EIP yatatolewa hadi Desemba 2020.
Je, muda wa mwisho wa kuwasilisha malipo ya kodi ni lini?
Muda wa mwisho kulipa kodi ya 2019 sasa ni Julai 15, 2020.
Kaya zenye kipata cha $69,000 au pungufu wanaweza kutumia IRS Free File mtandaoni.
Ikiwa utachelewa muda wa mwisho wa kulipa kodi Julai 15 kwa ajili ya kupata hundi ya kujikimu unaweza kupata fedha kama amana ya kodi utakapowasilisha malipo ya kodi ya 2020.
Je, nani hatapata hundi ya kujikimu hata kama watawasilisha malipo?
- Wategemezi wa walipa kodi, na watu ambao wanaweza kudaiwa kuwa ni wategemezi wa walipa kodi wengine. Hii inajumuisha wanafunzi wengi wa chuo.
- Wahamiaji wasio na Namba halali za Hifadhi ya Jamii.
- Ikiwa yeyote aliyeorodheshwa kwenye fomu yako ya kodi hakuwa na Namba halali ya Hifadhi ya Jamii, hautapata hundi.
Je, lini nitazipata fedha?
IRS inasema kwamba inapanga kuanza kutuma fedha mwishoni mwa Aprili, lakini itachukua wiki nyingi.
Je, wapi IRS itatuma fedha?
Ikiwa marejesho yako ya kodi au malipo yako ya Hifadhi ya Jamii yanawekwa moja kwa moja kwenye benki yako, IRS itaweka fedha kwenye akaunti hiyo hiyo ya benki. Vinginevyo, IRS itatuma fedha kwenye anwani iliyoorodheshwa kwenye fomu yako ya kodi ya hivi karibuni au kwenye maelezo ya mafao ya Hifadhi ya Jamii.
Ikiwa umehama hivi karibuni, sasisha anwani yako kwa kufanya hivi:
- Wasilisha malipo yako ya kodi ya 2019, kama bado hujafanya hivyo, au
- Wasilisha fomu ya mabadiliko ya anwani (fomu ya IRS namba 8822). Inaweza kuchukua wiki nne hadi sita IRS kushughulikia mabadiliko yako ya anwani, au
- Wasilisha mkondo wa kiotomatiki (fomu ya IRS namba 4868) pamoja na mabadiliko ya anwani.
Je, ninaweza kunyang'anywa hundi yangu ya kujikimu kwa sababu ya madeni?
Hundi yako ya kujikimu haitakabiliwa na fidia ya shirika la serikali kuu au la jimbo isipokuwa kitu kimoja: msaada wa watoto ambao haujalipwa. (Ikiwa unadhani unadaiwa msaada wa mtoto au hundi yako ya kujikimu imechukuliwa kwa ajili ya deni la msaada wa mtoto, piga simu Ofisi ya Msaada wa Mtoto wako ya jimbo kujua zaidi.)
Hata hivyo, Bunge halikutoa msamaha huu kwa ukusanyaji wa deni binafsi. Ikiwa utapata taarifa kutoka kwa mkopeshaji au benki yako kwamba wanajaribu kuchukua hundi yako ya kujikimu kupitia “mchakato wa wadhamini,” wasiliana nasi. Tunaweza kukuwakilisha na kueleza kuwa hawapaswi kuchukua hundi yako ya kujikimu. Benki yako pia inaweza kutumia hundi yako ya kujikimu ili kulipia malipo ya ziada na ada za benki ambazo unaweza kuwa unadaiwa. Ipigie simu benki yako ili kujua kama unadaiwa ada au gharama zozote na waulize watalishughulikiaje hilo.
Je, hundi ya kujikimu itaathiri mafao yangu?
Fedha za kujikimu hazitahesabika kama "mapato" na hazitapunguza mafao yako ya SSI, Reach Up, ruzuku ya makazi, Medicaid au 3SquaresVT (msaada wa chakula). Fedha hii pia haitahesabika kama "rasilimali" maadamu utaitumia ndani ya mwaka mmoja.
Nimesikia kuwa haya ni “malipo ya awali” ya marejesho ya kodi yangu ya 2020. Je, natakiwa kulipa ikiwa kipato changu cha 2020 ni kikubwa kuliko mwaka jana?
Hapana, IRS inategemea taarifa kutoka kwenye fomu zako za 2019 au 2018. Hakuna adhabu kwa kupata malipo ya awali makubwa kuliko vile ulivyotakiwa kupata. Ikiwa kipato chako halisi cha 2020 na idadi ya tegemezi inamaanisha ulipaswa kupata fedha zaidi, IRS itakulipa fedha za ziada mwaka 2021.
Nina maswali mengi kuhusiana na hali yangu. Je, nawezaje kupata msaada?
Wakazi wa Vermont wanaweza kuwasiliana nasi katika Kliniki ya Walipakodi wenye Kipato cha Chini ya Vermont (LITC) kwa kujaza fomu yetu au kwa kupiga simu 1-800-889-2047.