Taarifa Sahihi tangu 7/24/2020
Namba za simu za muhimu na kurasa za tovuti::
- Msaada wa Kisheria wa Vermont (VLA)/Huduma za Kisheria za Vermont (LSV) namba ya usajili: 1-800-889-2047
- Msaada/ Huduma za Kisheria za Vermont tovuti ya msaada wa kisheria ya Vermont: https://vtlawhelp.org/money-for-past-due-rent
- Makazi ya Dharura: Kituo cha Huduma za Mafao 1-800-479-6151 or 2-1-1
- Maombi ya Mpango wa Uimarishaji wa Makazi ya Kupangisha: https://www.vsha.org/rental-housing-stabilization-program/
- Chama cha Wamiliki wa Nyumba cha VT: 802-985-2764 or 888-569-7368
- Viwango vya Malipo vya VSHA: https://www.vsha.org/wp/wp-content/uploads/2020/07/Voucher-Payment-Standards.pdf
USTAHIKI
Nani anastahiki?
Kaya ambazo wamechelewa kulipa kodi zao za nyumba au kodi za kiwanja wanastahiki kwenye msaada wa kifedha. “Kaya” lazima lazima iwe wewe na familia yako, wewe na mnaoishi katik chumba pamoja. Unaitwa "mpangaji.”
Je, fedha zinaenda wapi?
Fedha zitalipwa moja kwa moja kwa wenye nyumba au wamiliki wa viwanja wa sasa au wa baadae, ikiwa wanakubali baadhi ya masharti. Fedha ni ruzuku ambayo haipaswi kurejeshwa.
Je, hali gani inastahiki kwa ajili ya ruzuku?
- Mpangaji anayedaiwa kodi pamoja na mwenye nyumba ambaye anahitaji kulipwa na kumbadikiza mpangaji.
- NDIO – Hali hii inastahiki kupata msaada.
- Mpangaji ambaye anahitaji amana ya ulinzi na kiasi cha malipo ya awali ya kodi kinachohitajika kumwamishia kwenye nyumba yenye gharama nafuu inatumika sawa na mwenye nyumba mpya ambaye yuko tayari kuwapangisha.
- NDIO – Hali hii inastahiki kupata msaada.
- Mwenye nyumba anadai kodi lakini mpangaji hajamjibu, na hajajibu maombi ya ruzuku ya kwenda VSHA.
- NDIYO – Mwenye nyumba anaweza kupata nusu ya kodi anayodai na akasitisha mkataba wa upangishaji. Mpangaji atapaswa kuhama baada ya mchakato wa kumfukuza mpangaji.
- Abiria wa Vermonter anayeishi kwenye moteli iliyolipiwa na Mpango wa Kuwanufaisha Watu wazima kwa miezi mingi tangu Machi, baada ya kufanya kazi na mpango wa kuingia ulioratibiwa.
- NDIYO – Piga Simu 211 au nenda kwenye helpingtohousevt.org kupata mpango wa kuingia ulioratibiwana kupata msaada.
Je, kuna ukomo wa mapato kupata fedha hizi?
Hapana. Hakuna kipimo cha mapato ili kupata msaada huu.
Je, ninapaswa kuwa nimepoteza mapato kwa sababu ya COVID kustahiki?
Hapana. Hupaswi kupoteza mapato kutokana na sababu zinazohusiana na COVID ili kupata msaada huu wa kifedha.
Ninakabiliwa na tatizo la kifedha kwa sababu ya COVID, lakini nimelipa kodi yangu kwa kutumia fedha za akiba au za kukopa. Je, ninastahiki?
Hapana. Ili kustahiki kupata msaada wa kudi ya nyuma kupitia mpango huu, wewe na mwenye nyumba wako mnatakiwa kuthibitisha kwamba kwa sasa kuna kodi inayodaiwa, na kwamba fedha inalipwa moja kwa moja kwa mwenye nyumba. Bahati mbaya, ikiwa umetumia fhedha nyingine na kwa sasa hudaiwi kodi, hustahiki kwenye ruzuku hii.
Ghorofa yangu inahitaji matengenezo. Je, ninastahiki?
Nyumba za kupangisha zinastahiki kupata msaada ikiwa zimekidhi Maadili ya Nyumba za Kupangisha za Vermonta au zitakidhi ndani ya siku 30. Ingawa, ikiwa nyumba ina ukiukaji wa viwango vya usalama wa maisha, fedha za kodi iliyopita haipatikani hadi ukarabati utkavyofanyika. Orodha ya ukiuka upo kwenye maombi na imejumuisha matatizo kama vile:
- kuvuja mafuta
- mafuriko
- hakuna maji moto
- hakuna choo
- matatizo ya umeme ambayo yanaweza kusababisha mstuko au moto
- n.k.
Katika maombi yako, ikiwa utatambua kwamba nyumba yako ina ukiukaji mkubwa wa viwango vya usalama wa maisha, utapelekwa kwa Afisa Afya wa serikali ya Mji na Msaada wa Kisheria wa Vermont.
Je, "ukosefu wa makazi" una maana gani katika muktadha huu?
Kwa madhumuni ya mpango huu, mtu anachukuliwa kuwa "hana makazi" ikiwa wamepata msaada wa dharura wa makazi kupitia DCF Economic Services (Huduma za Kiuchumi za DCF) katika mwezi wowote tangu Machi 2020.
Mwenye nyumba wangu tayari amefungua shauri la kunifukuza kwenye nyumba mahakamani. Je, bado ninastahiki?
Ndiyo. Hakika, ikiwa mwenye nyumba wako atapokea fedha za ruzuku, lazima atafuta shauri lolote la kukufukuza kwenye nyumba ambalo linasubiri kusikilizwa.
MAOMBI
Je, nawezaje kuomba kama mpangaji?
Tunapendekeza kwamba uanze kwa kuzungumza na mwenye nyumba kuhusu kuomba na kuthibitisha kiasi cha kodi kinachodaiwa. Kama mpangaji, unaweza kuomba kwa kupakua, kuhifadhi na kujaza maombi yanayopatikana yanayopatikana tovuti ya Mamlaka ya Nyumba ya Jimbo la Vermont (VSHA): https://www.vsha.org/wp/wp-content/uploads/2020/09/RHSP-Tenant-Application-9.3.20.pdf.
Mwenye nyumba wako lazima ajaze pia Uthibitisho wa Mwenye Nyumba unaopatikana kwenye tovuti ya VSHA: https://www.vsha.org/wp/wp-content/uploads/2020/09/RHSP-Landlord-Certification-9.3.20.pdf.
Kiasi cha kodi ya nyuma kinachodaiwa kilichoorodheshwa kwenye maombi haya yanapaswa kulingana. Mara baada ya Mamlaka ya Nyumba ya Jimbo la Vermont (VSHA) kupokea fomu zote mbili, itafanya maamuzi ndani ya siku 10.
Je, mwenye nyumba wangu ataambiwa kama nitatuma maombi?
Tunapendekeza kwamba uzungumze na mwenye nyumba yako kabla ya kuomba ili kuthibitisha kiasi cha kodi anadhani unadaiwa na kuuliza jina la kisheria la biashara la mwenye nyumba wako. Mwenye nyumba wako anapaswa kuwasilisha hati kabla ya maombi yako kukamilika. Ikiwa mwenye nyumba wako hataki kushiriki kwenye mpango, wasiliana na Msaada wa Kisheria wa Vermont kwa msaada.
Je, ninapaswa kuchapisha na kusaini maombi haya?
Hapana, unaweza kuandika jina lako kwenye mstari wa sahihi badala ya kuchapisha na kuisaini hati. Hakikisha unapakua na kuhifadhi maombi kwenye kompyuta au kwenye vifaa vingine kabla ya kuyajaza. Mara baada ya kuijaza, unaweza kuituma kwenda rentrelief@vsha.org.
Ikiwa chumba natumia na watu wengine, je, kila mmoja anapaswa kuomba?
Ikiwa kaya yako ina mkataba mmoja wa upangishaji na mwenye nyumba, unapaswa kuwasilisha maombi mara moja ambayo yanajumuisha kodi zote zinazodaiwa kwa kaya nzima.
Je, mwenye nyumba anatumaje maombi?
Kutuma maombi, mwenye nyumba lazima ajaze fomu ya uthibitisho, fomu ya kuweka fedha moja kwa moja na fomu ya W-9. Zote zinapatikana kwenye tovuti ya VSHA: https://www.vsha.org/rental-housing-stabilization-program/. Pia lazima awape VSHA hundi wazi. Chama cha Wenye Nyumba cha VT (802-985-2764 or 888-569-7368) kinatoa msaada kwa wenye nyumba ambao wanatuma maombi.
Ikiwa mpangaji anatuma maombi, je, mwenye nyumba anapaswa kushiriki? Je, itakuwaje ikiwa hawatashiriki?
Wenye nyumba anaweza kuamua kutoshiriki katika mpango huu. Ushiriki unawataka wao kukubaliana na baadhi ya mambo kama vile kusamehe ada ya kuchelewa kulipa na kuto mfukuza mpangaji kwenye nyumba kwa kutolipa kwa muda fulani. Wanaweza kuamua kutokubaliana na masharti hayo. Ikiwa unadaiwa kodi ya nyuma na unakabiliwa na kufukuzwa kwenye nyumba, unaweza kuwasiliana na nasi kupitia Msaada wa Kisheria wa Vermont kwa 1-800-889-2047 kwa ajili ya ushauri.
Je, napaswa kufanya nini ikiwa sina makazi?
Ikiwa unatuma maombi ya fedha ili kukusaidia kwa ajili ya amana ya ulinzi na kodi ili kuhamia, wewe na mwenye nyumba wako mtarajiwa mnapaswa kutuma maombi. Maombi yanapaswa yaseme:
- kiasi cha amana ya ulinzi, na
- kiasi cha malipo ya awali ya kodi kinachohitajika ili kuhamia.
Kiasi hiki kinapaswa kuwa sawa kwenye maombi yote mawili.
Ikiwa huna makazi na unahitaji ruzuku inayoendelea ya kodi, VSHA watakwambia ushirikiane kwanza na Uingiaji Ulioratibiwa. Pida simu 211 au nenda kwenye helpingtohousevt.org ili kupata mpango wa uingiaji ulioratibiwa.
Je, inamaana gani kwa upangaji kuwa "sio endelevu"? Je, nani anapaswa kuchagua kisanduku hicho kwenye maombi?
Upangaji wako "sio endelevu" ikiwa — bila kujali mapato au mabadiliko ya matumizi kwa sababu ya COVID-19 —nyumba yako ya sasa ilikuwa ghali kwa kaya yako. Unaweza kuwa katika hali hii ikiwa umepata nyumba ya gharama nafuu zaidi, lakini unahitaji fedha kwa ajili ya amana ya ulinzi na kiasi cha malipo ya awali ya kodi inayohitajika ili kuhamia.
Ikiwa una mapato ya chini sana na huwezi kupata nyumba ya gharama nafuu sana, piga simu 211 au nenda helpingtohousevt.org. Unaweza kupata hirika lakukusaidia kupata mafao ya makazi hivyo utaweza kumudu gharama za makazi.
Je, fomu zinapatikana kwa lugha nyingine zaidi ya Kiingereza?
Kwa sasa fomu zinapatikana kwa Kiingereza tu, lakini hivi karibuni zitapatikana kwa lugha nyingine. Mamlaka ya Nyumba ya Jimbo la Vermont (802-828-3295) watakuwa na wakalimani. Ikiwa unakabiliwa na matatizo kutuma maombi, wasiliana na Msaada wa Kisheria wa Vermont (1-800-889-2047) na pia tutakuwa na wakalimani.
Nifanyaje ikiwa nina maswali kuhusu maombiu?
Mpangaji ambaye anahitaji msaada wa maombi anaweza kuwasiliana na namba ya usajili ya Msaada wa Kisheria wa Vermont: 1-800-889-2047. Kwa taarifa zaidi kuhusu mpango, ikiwemo Maswali Yanayoulizwa Sana, vinapatikana kwenye tovuti ya VSHA: https://www.vsha.org/rental-housing-stabilization-program/. Tovuti yetu ya msaada wa kisheria pia ina baadhi ya taarifa: https://vtlawhelp.org/money-for-past-due-rent
KIASI
Fedha kiasi gani kwa kodi ya nyuma nayodaiwa ninayoweza kupata?
Kwa kila mwezi ambao unadaiwa kodi, VSHA watamlipa mwenye nyumba wako ama kiasi unachodaiwa au kiwango cha malipo cha VSHA—chochote ambaocho ni kidogo. Ikiwa mwenye nyumba atakubali fedha za ruzuku, huna haja ya kulipa ada yoyote ya kuchelewa kulipa au kiasi unachodaiwa kilichozidi kiwango cha malipo.
Je, itakuwaje ikiwa kodi yangu ya kila mwezi ni kubwa kuliko kiwango cha malipo ya VSHA?
Kwa kubali fedha za ruzuku, mwenye nyumba yako amekubaliana na kupokea kiasi cha juu cha kiwango cha malipo cha VSHA kwa kila mwezi, hata kama unadaiwa zaidi ya kiasi hicho. Huna haja ya kulipa kiasi chochote unachodaiwa kilichozidi kiwango cha malipo.
Mwenye nyumba wangu hatakubali kujaza makaratasi isipokuwa kama nitalipa fedha za ziada kwa upande wangu. Je, nitafanyaje?
Malipo ya pembeni hayaruhusiwi kwa mujibu wa mpango huu. Mwenye nyumba wako hapaswi kukuhimiza kwamba ulipe zaidi ya kiwango cha malipo cha VSHA kwa kila mwezi. Ikiwa mwenye nyumba hatakubaliana na masharti ya mpango, wasiliana na Msaada wa Kisheria wa Vermont kwa namba 1-800-889-2047. Hakikisha unawasiliana nasi ikiwa umepata tangazo la kusitisha mkataba au nyaraka kuhusu shauri la mahakamani.
Sina makazi. Je, kiasi gani cha fedha ninachoweza kupata ili kinisaidie kupata makazi mapya?
Ikiwa ulikaa kwenye nyumba iliyolipiwa na Mpango wa Kuwasaidia Watu Wazima muda wowote tangu Machi, unaweza kustahiki kupata amana ya ulinzi na kodi ya kwanza na ya mwisho. Kutuma maombi, wewe na mwenye nyumba wako ajaye lazima wote mtume maombi. Maombi yako lazima yaseme:
- kiasi cha amana ya ulinzi, na
- kiasi gani cha malipo ya awali ya kodi kinahitajika ili kuhamia.
Maombi yako yatatumwa kwenda Shirika la Vermont la Huduma za Binadamu kwa ajili ya msaada, au unaweza kuwasiliana na shirika la uingiaji ulioratibiwa la mahali ulipo. Piga simu 211 au nenda helpingtohousevt.org ili kupata mpango wa uingiaji ulioratibiwa.
NYINGINE
Je, ninaweza kupata fedha hizi ikiwa mimi si raia? Itakuwaje ikiwa Sipo katika nchi hii na hadhi ya Kisheria?
Mpango wa uimarishaji nyumba za kupangisha unapatikana kwa kila mtu ambaye kwa sasa anapanga katika Jimbo la Vermont bila kujali uraia au hadhi ya uhamiaji.“
Ikiwa tumeidhinisha na mwenye nyumba amepata fedha, je, hilo linaweza kunilinda nisifukuzwe kwenye nyumba? Kwa muda gani?
Ikiwa mwenye nyumba wako amekubali fedha, lazima aondoe hati yoyote ya kukufukuza inayosubiri utekelezaji, kusamehe ada zote za kuchelewa kulipa, na kuchukulia kodi yako ya nyuma inayodaiwa kuwa imelipwa kikamilifu kwa miezi yoyote iliyogharamiwa na ruzuku. Mwenye nyumba wako pia anakubali kutomfukuza mpangaji kwa sababu ya kutokulipa kodi kwa miezi mingi au kwa miezi 6, chochote kilichokidogo. Hata hivyo, mwenye nyumba wako anaweza kukufukuza kwenye nyumba "kwa sababu" (kwa mfano, ikiwa umekiuka sana kanuni za mkataba wako wa kupanga) ikiwa suala jipya litajitokeza baada ya ruzuku kulipwa. Ikiwa mwenye nyumba atakubali fedha za kodi ya nyuma, na hafuati kanuni, mwenye nyumba anapaswa kuzilipa fedha hizo
Je, hizi fedha zinahesabika kama mapato ambayo yanaweza kuathiri kipimo cha mafao au kwenye kodi yangu?
Fedha hizi zinalipwa moja kwa moja kwa mwenye nyumba. Inapunguza gharama zako za nyumba. Ikiwa mpango wa mafao unahesabia gharama za nyumba unayolipa, itaathiri mafao yako. Ikiwa mpango wako wa mafao hauhesabii gharama za nyumba, haitaathiri. (Mfano: Medicaid haihesabii gharama za nyumba, hivyo hilo haliwezi kuathiri Medicaid.)
Je, ni kwa jinsi gani Msaada wa Kisheria wa Vermont unanisaidia kwa hili?
Kila mtu anapaswa kujaribu kuanza mchakato huu kwa:
- kuwasiliana na mwenye nnyumba wako
- kuthibitisha kiasi kinachodaiwa, na
- kutuma maombi.
Ikiwa huna kompyuta au simu janja, uliza kama mwenye nyumba wako ata tuma maombi pamoja na wewe na tumia kompyuta yake. Au tumia kompyuta ya rafiki. Ikiwa utakabiliwa na tatizo wakati wa mchakato huo, wapigie simu Msaada wa Kisheria wa Vermont. Au, ikiwa huna uhakika wa kile unachopaswa kukijumuisha kwenye maombi, unaweza kuwasiliana nasi pia. Piga simu 1-800-889-2047.
Je, kuna faida zozote za kusubiri kutuma maombi, ili niweze kupata msaada wa miezi mingi zaidi ya kodi?
Mpango huu ni anayewahi, ndiye anayepata, pamoja na kiasi kamili cha fedha. Unapaswa kutuma maombi yako haraka uwezavyo. Ikiwa utachelewa kulipa kodi yako tena kabla ya mwaka kuisha, basi unaweza kutuma maombi kwa ajili ya msaada tena.
Ninahitaji msaada wa rehani yangu.
Shirika la Fedha za Nyumba la Vermont linaendesha mpango huu kwa ajili ya fedha za msaada wa rehani. Maombi yapo kwenye tovuti ya Shirika la Fedha za Nyumba la Vermont (VHFA): http://www.vhfa.org/map.