KUMBUKA: Taarifa hii ilikuwa sahihi hadi Aprili 17, 2020, hata hivyo baadhi ya taarifa zinaweza kuwa zimebadilishwa kuanzia hapo. Tafadhali angalia vtlawhelp.org kwa taarifa mpya zozote.
Ikiwa umepoteza kazi yako au saa zako za kazi zimepunguzwa kwa sababu ya virusi vya korona vya COVID-19, labda unaweza kupata msaada fulani. Unaweza kutuma maombi ya mafao hata kama mwajiri wako anasema usifanye hivyo. Waajiri hawafanyi maamuzi kuhusu mafao ya ukosefu wa ajira — serikali ya jimbo inaweza kufanya hivyo.
Je, ninastahiki mafao ya ukosefu wa ajira wakati wa janga la COVID-19?
Unapaswa kutuma maombi ikiwa:
- ulikuwa umefutwa kazi
- ulipewa likizo
- saa zako za kazi zilipunguzwa
- uliajiriwa lakini hukuanza kufanya kazi kwa sababu ya COVID-19
- ulipaswa kuacha kazi ili kulea mtoto ambaye shule au kituo chake cha kulea watoto kilifungwa kwa sababu ya COVID-19
- alipaswa kuacha kazi ili kuhudumia mwanakaya aliyekutwa na maambukizi ya COVID-19
- alipaswa kukaa karantini kufuata maelekezo ya daktari
- alikutwa na maambukizi ya COVID-19 au ana dalili na anahitaji vipimo
- hawezi kufanya kazi kwa sababu ya amri ya kukaa nyumbani
- ulimwomba mwajiri wako kufanya kazi ukiwa mbali kwa sababu za kiafya na mwajiri wako alisema "hapana"
- uliacha kazi kwa sababu mwajiri wako hakufuata miongozi ya usalama na alikuweka kwenye hatari kubwa ya kupata COVID-19
Kama huwezi kufanya kazi kwa sababu upo karantini, unaumwa, unamuuguza mwanafamilia ambaye anaumwa, au unamlea mtoto, unapaswa kuangalia kama unastahili malipo ya Vermont ya wakati wa kuumwa na likizo yenye malipo ya COVID-19 ya serikali kuu. Fanya hivi kabla ya kutuma maombi ya fao la ukosefu wa ajira. Angalia ukurasa wetu kuhusu sheria mpya ya serikali kuu ya likizo yenye malipo.
Kumbuka, haijalishi kama mwajiri wako anasema "haujafutwa kazi" au "haujapewa likizo." Serikali ya jimbo inaamua iwapo sababu kuacha kazi inafanya ustahili kwa ajili ya fao la ukosefu wa ajira, sio mwajiri wako.
Je, mimi ninastaki hata kama ni “mfanyakazi wa mtandaoni” au kontrakta anayejitegemea?
Ndio! Ikiwa umejiajiri, kontrakta wa kujitegemea au mfanyakazi huria unaweza kustahiki ikiwa unakidhi vigezo vingine vilivyoorodheshwa hapo juu.
Vermont bado inaweka kanuni na mchakato wa maombi kwa ajili ya fao hili. Vinjari tovuti ya Wizara ya Kazi ili kuwajulisha jinsi ya kuwasiliana na wewe pale maombi haya yatapokuwa teyari.
Kumbuka: Je, biashara yako ndogo imetuma maombi ya "Ulinzi wa Malipo" mkopo wa SBA au mkopo wa majanga ya majeraha ya kiuchumi? Je, msaada huu unakuruhusu kudumisha saa za kawaida? Kama ndio, basi labda huwezi kupata fao la ukosefu wa ajira chini ya mipango mipya.
Je, inakuaje ikiwa sikutimiza kiwango cha chini cha mahitaji ya historia ya kazi mwaka huu?
Ndio! Hata kama huna historia muhimu unaweza kupata mafao ya ukosefu wa ajira katika kipindi hiki.
Je, mimi ninastahiki ikiwa sio raia wa Marekani?
Hasa, ikiwa wewe sio raia wa Marekani, unastahiki kwa fao la ukosefu wa ajira ikiwa una kibali halali cha kufanya kazi Marekani kwa sasa na ulikuwa nacho ulipokuwa unafanya kazi. Mradi wa Sheria ya Ajira wa Taifa una muhtasari wa kile tunachokijua, na tusichokijua, kuhusu kustahiki kwako kwenye mafao ya ukosefu wa ajira kwa wakati huu.
Wahamiaji wasiokuwa na hati hawawezi kupata mafao ya ukosefu wa ajira.
Je, unaishi Vermont? Je, una maswali kuhusu hali yako ya uhamiaji au kibali chako cha kufanya kazi Marekani? Wasiliana na AALV au Kliniki ya Sheria ya South Royalton.
Je, kiasi gani cha fedha ninaweza kukipokea kila wiki?
Kwa kawaida serikali ya jimbo inakadiria kiasi cha fao lako la kila wiki kwa kutumia kanuni hii. Kiasi kikubwa kabisa cha fao ni $513/wiki.
Ikiwa sasa unastahili fao la ukosefu wa ajira kwa sababu ya COVID-19 (kwa mfano, kwa sababu huna historia kubwa kazi au wewe ni kontrakta wa kujitegemea), Vermont bado inaandika kanuni za jinsi fao lako litakokotolewa. Kiasi kitakuwa kati ya $191/wiki (nusu ya wastani wa fao la ukosefu wa ajira la jimbo katika robo ya mwisho) na $513/wiki.
Ikiwa unawasilisha madai ya kila wiki utapata ziada ya $600 ya "fidia ya ukosefu wa ajira iliyosababishwa na janga” kila wiki. Fedha hii inapatikana hadi Julai 31, 2020. Unaweza kuipata hata kama unapokea sehemu ya fao la kukosa ajira.
Je, ni kwa kipindi gani ninaweza kupata mafao ya bima ya ukosefu wa ajira wakati wa majanga?
Kama unastahili, unaweza kupata mafao ya ukosefu wa ajira kwa hadi wiki 39 au hadi Decemba 31, 2020 -- chochote kitakachoanza.
Itakuwaje ikiwa teyari nilitumia hadi wiki zangu 26 za ukosefu wa ajira mwaka huu?
Ikiwa umewasilisha madai mengine na unastahiki, unaweza kupata wiki zingine 13 za ziada za mafao ya ukosefu wa ajira. Hakikisha unawasilisha tena maombi kwa ajili ya hili.
Je, taarifa gani ninahitaji ili kutuma maombi?
Angalia kwenye orodha chini ya ukurasa huu kwenye tovuti ya Wizara ya Kazi. Andaa taarifa nyingi kadri uwezavyo.
Jaji katika Wizara ya Kazi anaweza kuwasiliana na wewe na/au mwajiri wako ikiwa:
- taarifa imekosekana, au
- wewe na mwajiri wako hamkubaliani kuhusu jambo lolote la maswala haya.
Jitahidi uwezavyo kumsaidia jaji kupata taarifa wanazohitaji. Waambie ikiwa huwezi kuzifikia taarifa zozote kati ya hizi.
Je, ninatumaje maombi?
Jimboni Vermont, madai ya awali ya fidia ya ukosefu wa ajira lazima yafanyike kwa simu au mtandaoni. Piga simu 1-877-214-3330 au 1-888-807-7072. Wazira ya Kazi ya Vermont ina fomu ya mtandaoni. Jaza fomu hapa.
Ikiwa wewe ni kontrakta wa kujitegemea, umejiajiri au mfanyakazi wa mtandaoni, inaweza kuwa wiki chache kabla ya kuweza kuwasilisha madai yako. Vermont bado inaweka kanuni na mchakato wa maombi kwa ajili ya fao hili. Vinjari tovuti ya Wizara ya Kazi ili kuwajulisha jinsi ya kuwasiliana na wewe pale maombi haya yatapokuwa teyari.
Kabla ya kuwasiliana na Wizara ya Kazi ili kuwasilisha madai, kusanya taarifa kutoka kwenye orodha yao ya taarifa zinazohitajika. Wizara ya Kazi inashughulikia simu nyingi hivyo inaweza kuchukua muda mrefu kuzungumza kwa simu.
Je, muda gani natakiwa kusubiri?
Kwa sasa, Wizara ya Kazi haina kipindi cha kusubiri kwa ajili ya mafao ya ukosefu wa ajira.
Katika nyakati za kawaida, kawaida inachuku karibia wiki mbili kupata malipo yako ya kwanza. Kwa sababu ya janga, unaweza kusubiri muda mrefu zaidi. Si rahisi kujua haswa muda gani utapata malipo yako ya kwanza.
Je, napaswa kufanya jambo lolote baada ya kuwa nastahiki?
Endelea kuwasilisha madai yako kila wiki ambayo huwezi kufanya kazi au saa zilizopunguzwa. Ikiwa jina lako linaanza na A-E, wasilisha madai yako ya kila wiki Jumatatu, F-L Jumanne, M-R Jumatano na S-Z Ijumaa.
Hadi Wizara ya Kazi itakaposema vinginevyo, huhitaji kuthibitisha kwamba unatafuta kazi. Wizara ya Kazi hataki watu kuathiri afya zao au afya za wengine wakati huu wa janga la virusi vya korona. Haulazimiki kuonyesha kwamba umepata usaili wa kazi, umehudhuria maonyesho ya kazi, na kadhalika.
Je, hii itaadhilije mafao yangu, makazi, na huduma yangu ya afya?
Ikiwa unapata msaada wa serikali kama vile 3SquaresVT (msaada wa chakula), msaada wa mafuta, Msaada wa Jumla, Reach-Up, au SSI, unapaswa kutoa taarifa ya fedha unazopata kutokana na ukosefu wa ajira kwa kila moja ya mpango. Hasa unapaswa kutoa taarifa ya fedha ndani ya siku 10 ulipoanza kupata mafao ya ukosefu wa ajira. Mafao yako mengine yanaweza kupunguzwa au kusitishwa unapopokea mafao ya ukosefu wa ajira, kutegemeana na kiasi unachopata kwenye mafao ya ukosefu wa ajira.
Pia unapaswa kutoa taarifa ya kila moja ya mipango hii pale unapokuwa hustahiki kwenye mafao ya ukosefu wa ajira, ili uweze kurudishiwa 3SquaresVT, msaada wa mafuta, Msaada wa Jumla, Reach-Up, na SSI zako.
Ikiwa unaishi nyumba yenye ruzuku, unapaswa kutoa taarifa mafao yako ya ukosefu wa ajira kwa mwenye nyumba wako (ikiwa unaishi kwenye jengo lenye ruzuku) au mamlaka yako ya makazi (ikiwa umepata msaada wa kodi ya pangokama vile vocha ya Kifungu cha 8). Sehemu yako ya kodi inaweza kuongezeka wakati unapopata mafao ya ukosefu wa ajira. Pia unapaswa kutoa taarifa wakati mafao yako ya ukosefu wa ajira yanapo koma, ili sehemu yako ya kodi ya pango itapungua tena.
Medicaid pia inahesabika kwenye fedha hii ya ukosefu wa ajira, isipokuwa $600/wiki katika “fidia ya ukosefu wa ajira uliosababishwa na janga.” Unatakiwa utoe taarifa ya fedha zako za ukosefu wa ajira kwa Medicaid ya Vermont. Tunadhani watu wengi wataweza kupata mafao ya ukosefu wa ajira ya ziada na kuendelea na Medicaid zao. Ikiwa utapata barua inayosema Medicaid yako inabadilika au inamalizika, tafadhali wasiliana nasi katika Ofisi ya Wakili wa Huduma ya Afya (HCA). Piga simu 1-800-917-7787 ili kuzungumza na wakili wa huduma ya afya, au jaza Fomu yetu ya Kuomba Msaada. HCA ni bure kwa Wavermont.
Je, nini kinatokea ikiwa nitakataliwa?
Una siku 30 toka tarehe iliyoandikwa kwenye tangazo kukata rufaa. Lakini kukataliwa kungine kunaweza kusuluhishwa bila ya kukata rufaa. Wizara ya Kazi inashughulikia maombi mengi hivi sasa, na karibia nusu ya waombaji wanakataliwa kwa mara ya kwanza kwa sababu mfumo hauna taarifa za kutosha. Kabla ya kukata rufaa, unaweza kujaribu kuwasiliana na Wizara ya Kazi siku uliyopangiwa ili kuona ikiwa wewe ni miongoni mwa watu ambao madai yao yanaweza kutatuliwa. Ikiwa jina lako la mwisho linaanza na A-E, piga simu Jumatatu, F-L Jumanne, M-R Jumatano na S-Z Ijumaa.
Tunaweza kukusaidia kuamua ikiwa unahitaji kukata rufaa ya kukataliwa kwako mafao ya ukosefu wa ajira au la. Jaza fomu yetu na tutakupigia simu. Taarifa zako zitaenda kwenye Huduma za Sheria za Vermont, ambayo wanachunguza maombi kwa kusaidiana na Msaada wa Kisheria wa Vermont na Huduma za Sheria za Vermont. Pia unaweza kutupigia simu kwa 1-800-889-2047.
Ikiwa inabidi kukata rufaa, hakikisha unatuma barua kwenda Wizara ya Kazi ndani ya siku 30 ya tarehe ya kukataliwa au "barua ya uamuzi." Waambie unataka kukata rufaa. Pia unaweza kutuma rufaa yako kwa barua pepe, faksi au kuweka kwenye sanduku la barua laki japokuwa umeituma, inatakiwa iwe ndani ya siku 30 ya tarehe ya barua ya kukataliwa. Angalia tovuti ya Wizara ya Kazi kwa maelezo zaidi ya kitu cha kujumuishwa katika barua ya rufaa. Hifadhi nakala ya barua.
Ikiwa utatumia fomu ya rufaa, unaweza kutumia fomu ya Rufaa ya Mlalamikaji ya UI. Ijaze na uhihifadhi nakala yako.
Jaji wa Sheria ya Utawala (ALJ) atapitia madai na kukataliwa kwako na rufaa itasikilizwa kwa njia ya simu. Angalia nyuma ya Tangazo la Usikilizaji Shauri au tovuti ya Wizara ya Kazi kwa maelezo zaidi kuhusu mchakato wa rufaa.
????
More in Kiswahili / Swahili: Audio about COVID-19 financial help from CVOEO